Story by Our Correspondents –
Waziri wa Elimu nchini Prof. George Magaho amesema serikali haina mipango ya kuondoa mfumo mpya wa elimu wa CBC shuleni bali utaendelea kutekeleza.
Akizungumza na Wanahabari jijini Nairobi, Waziri Magoha amewapuuzilia mbali wale wanaodai kwamba mfumo wa CBC ni mzigo mkubwa kwa wazazi, akisema ni lazima wazazi wawe tayari kuupokea mfumo huo.
Waziri Magoho amesema jinsi baadhi ya watu wanavyoendeleza shinikizo za kuondolewa kwa mfumo huo mpya wa elimu na wengine wakielekea Mahakamani ni njama za siasa na wala hawana malengo bora kwa wanafunzi.
Wakati uo huo amewataka wazazi kutokubali kuhadaiwa na baadhi ya watu wachache wasiopenda maendeleo ya watoto shuleni, akisema ni lazima taifa hili lishuhudie mabadiliko ndipo litapiga hatua kimaendeleo.