Picha kwa hisani –
Waziri wa Elimu nchini Profesa George Magoha, amesema serikali kwa sasa haina mipango ya kuzifunga tena shule licha ya idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini kuongezeka.
Waziri Magoha amesema zaidi ya wanafunzi milioni 3 wa gredi ya nne, darasa la nane na kidato cha nne wamerudi shuleni katika awamu ya kwanza ya ufunguzi wa shule na wazazi hawafai kuwa na wasiwasi wowote.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kufanya ziara ya kielimu katika maeneo ya Mumis na Malaba, Magoha amesema Wizara ya Elimu inashirikiana na ile ya usalama wa ndani kutathmini hali halisi ya maeneo ya shule.
Waziri Magoha ameshikilia kuwa hakuna anayefirikia kufunguliwa kwa shule wala kuzifunga shule hizo lakini uamuzi mwafaka utafanywa kuwa kuzingatia ukweli.
Wakati uo huo amepinga madai yalioibuliwa kwa kuna baadhi ya shule zimekosa kufanya mitihani ya majaribio, akisema mikakati yote imeandaliwa na wanafunzi wote wa gredi ya nne, Darasa la nane na wale wa kidato cha nne walio shuleni watashirikia mitihani hiyo ya majaribio.