Picha kwa hisani
Waziri wa Elimu nchini Profesa George Magoha amewaagiza wasimamizi wa shule zote za msingi na upili nchini, kuwarudishia wazazi ambao tayari walikuwa wamelipa karo za muhula wa pili na watatu, akisema wanafunzi hawajakuwa shuleni.
Waziri Magoha, amesema kora hizo zinaweza pia kutumiwa mwaka ujao lakini kwa maelewano kati ya wazazi na wasimamizi wa shule hizo huku akisisitiza kuwa shule zitafunguliwa mwaka ujao.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kufanya ziara ya kielimu katika kaunti ya Taita taveta, Magoha ameondoa utata uliokuwa unawakumba wazazi kuhusu wanafunzi wanaofaa kujiunga na shule kwa mara ya kwanza kamba wanaweza kusoma kwa zamu.
Kauli ya Waziri Magoha imejiri siku moja tu baada ya kutangaza kuwa shule zitafunguliwa mwezi Januari mwaka ujao huku mitihani ya kitaifa mwaka huu ya KCPE na KCSE ikihairishwa.