Wizara ya Elimu nchini ametoa agizo kwa wasimamizi wa shule za msingi na upili nchini kuhakikisha zinawalinda vyema wanafunzi wakati huu ambapo shule zimeagizwa kufungwa.
Wizara hiyo kupitia Waziri George Magoha, imewaagiza wasimamizi wa shule hizo kuhakikisha mabasi ya shule yanawapeleka wanafunzi hadi majumbani mwao ama maeneo yaliosalama kwa wanafunzi hao kufika nyumbani.
Waziri Magoha amesema agizo hilo linafaa kutekelezwa kikamilifu ili kuzuia wanafunzi kuambukizwa virusi vya Corona, kwani wengi wao bado hawajafaa jinsi ya kujikinga.
Kauli ya Magoha amejiri kutokana na wasiwasi uliowaingia wazazi baada ya serikali kutangaza kuthibitishwa kwa visa viwili vya Corona nchini huku Shirika la Afya duniani WHO likitangaza kuwa zaidi ya watu laki moja na elfu 30 wameambukizi virusi hivyo katika mataifa 118.