Story by Our Correspondents –
Zaidi ya watahiniwa milioni 2.5 kote nchini wa darasa la nane KCPE na wale wa gredi ya sita KPSEA wameanza rasmi mitihani yao ya kitaifa na Somo la Hesabati, kisha baada ya wakafanya somo la Kiingereza na kumalizia siku ya leo na somo la Insha ya Kiingereza.
Kulingana na wadau wa sekta ya elimu nchini, maandalizi ya mitihani hiyo ilifanyika vyema na wanafunzi hawafai kuhofia lolote na badala yake wajitahidi kufanya vyema mitihani hiyo.
Waziri wa Elimu nchini Ezekiel Machogu amefanya ziara ya kielimu kanda ya Pwani na kushuhudia ukaguzi wa kasha la mitihani hiyo katika shule ya msingi ya Mvita kaunti ya Mombasa.
Waziri Machogu amewahakikishia wanafunzi na wazazi sawa na wadau wa elimu kwamba mitihani hiyo itapewa ulinzi wa kutosha na kuwaonya wanafunzi na wazazi dhidi ya kushiriki udanganyifu.