Picha kwa hisani –
Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe amejitenga na sakata ya ubadhirifu wa fedha za umma zilizotengewa Shirika la usambazaji wa dawa nchini KEMSA, kushuhulikia janga la Corona.
Akijitetea mbele ya Kamati ya bunge la kitaifa kuhusu Afya inayoongozwa na Sabina Chege, Waziri Kagwe amesema ni jukumu lake kama Waziri kushinikiza kuwepo na uwajibikaji katika Wizara hiyo huku akidai kuwa sio jukumu lake kuwaambia watu washiriki uhalifu.
Waziri Kagwe ameweka wazi kuwa ni jukumu lake kutoa muongozo wa kikazi na wala sio kuhusika katika sakata ya uporaji wa fedha za umma ambapo shilingi bilioni 5 zinadaiwa kutumika kimakosa katika ununuzi wa vifaa vya kupima Corona.
Wizara huyo, amejitenga pia na madai ya kushirikiana na mashirika ya kibinafsi katika kusambaza vifaa vya kujikinga na Corona, akisema Shirika la KEMSA linafaa kutumia vifaa iliovyo navyo na wala sio kuitisha fedha zaidi.
Katika kikao hicho, Mwakilishi wa Kike kaunti ya Lamu Bi Ruweda Obo ametaka ufafanuzi zaidi kuhusiana na sakata hiyo hasa katika risiti za ununuzi wa vifaa vya Corona.
Akijubu maswala yaliouweza na wabunge katika kikao hicho, Katibu katika Wizara hiyo Susan Mochache amejitenga na sakata hiyo, akidai kuwa Wizara ya Afya haihusiki kivyovyo na uagizaji wa vifaa vya kiafya bali Wizara hiyo iliopokea utarajibu kutoka Shirika la KEMSA.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Sabina Chege ameagiza kuzingatiwa kwa agizo la Rais Uhuru Kenyatta katika kutangaza zabuni kupitia wavuvi ili kuwepo na uwazi katika ununuzi wa bidhaa mbalimbali nchini.