Story by Our Correspondents –
Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe amewahimiza wakenya kutopuuza zoezi la kujisajili kama wanachama wa hazina ya kitaifa ya bima ya matibabu NHIF, akisema itawasaidia katika kupata matibabu bila ya changamoto.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuzindua kituo cha mafunzo ya Sayansi katika Hospitali ya PECA Chogoria katika kaunti ya Tharaka Nithi, Kagwe amesema mabadiliko kadhaa yanaendelea katika hazina hiyo ili kuboresha huduma zake.
Kagwe amesema mabadiliko hayo yatachangia wakenya wengi kunufaika na huduma za bima ya NHIF kwani idadi kubwa ya wakenya wamekuwa wakipitia changamoto wakati wakitafuta huduma za matibabu.
Wakati uo huo Wizara ya Afya nchini imedokeza kwamba watu 54 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona baada ya sampuli 5,578 kufanyiwa uchunguzi na idadi hiyo kuongezeka hadi watu 322,388.
Hata hivyo wagonjwa wa Corona 2,342 wametangazwa kupona virusi hivyo na kuchangia idadi hiyo kufikia watu 302,647 huku wale walioaga dunia kutokana na makali ya Corona ikifikia watu 5,626.