Picha kwa hisani –
Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe amewahimiza wakenya kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, akisema virusi hivyo vimeenea kila mahali nchini.
Waziri Kagwe, amewaonya wakenya dhidi ya kupuuza masharti ya kiafya yaliowekwa na serikali ya kujikinga na Corona, akisema ni lazima kila mkenya kuwa muuangalifu na kuwalinda wazazi dhidi ya maambukizi.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kufanya ukaguzi wa kiafya katika hospitali kuu ya Kenyatta jijini Nairobi, Waziri Kagwe amesisitiza muhimu wa wakenya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona sawia na kuzingatia masharti ya kiafya.
Akigusia takwimu za maambukizi ya virusi vya Corona, Waziri Kagwe amesema idadi ya watu wanaliofariki kutokana na maambukizi hayo imefikia watu 391 baada ya watu 3 kuaga dunia.
Kagwe amesema watu 671 wamethibitishwa kupata maambukizi hayo kutokana na sampuli 6,200 na idadi hiyo kuongezeka hadi watu 23,873.
Wakati uo huo amedokeza kuwa watu 603 walikuwa wakiugua virusi hivyo wamepona na kupelekea idadi ya waliopona nchini kufikia watu 9,930.