Story by Mwanaamina Fakii –
Wizara ya Afya katika kaunti ya Kwale imewahimiza wakaazi wa kaunti hiyo kuzingatia umuhimu wa kutumia vyoo kwani hatua hiyo itachangia uimarishaji wa usafi katika jamii.
Waziri wa Afya katika serikali ya kaunti ya Kwale Francis Gwama amesema utumizi wa vyoo hudhibiti mlipuko wa magonjwa mbalimbali kwani jamii itakuwa inadumisha usafi.
Gwama amesema licha ya jamii kukumbwa na changamoto za maisha, Wizara hiyo imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na jamii ili kujenga vyoo.
Hata hivyo amedokeza kwamba mara nyingi magonjwa yanayotokana na ukosefu wa vyoo huwa ni kuharisha, miyoo, upungufu wa damu na magonjwa ya kifuu, akisisitiza umuhimu wa jamii kuzingatia ujenzi wa vyoo.