Waziri wa Utalii nchini Najib Balala amewahimiza wakenya kukumbatia utalii wa kinyumbani, akisema hatua hiyo itasaidia kuenua sekta ya Utalii ambayo imesambaratika kufuatia janga la Corona.
Kwenye ujumbe wake kwa wakenya wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Utalii ulimwengu, Waziri Balala amesema wakenya wanafaa kushirikia ili kufufua sekta hiyo.
Balala amesema sekta ya Utalii kote ulimwenguni ikiwemo nchini Kenya imezorota kufutia mataifa mbalimbali kusitishwa safari za moja kwa moja ndege kufuatia mlipuko wa janga la Corona.
Wakati uo huo Waziri Balala amewapa changamoto Magavana wa kaunti zote 47 nchini kuhakikisha wanaibuka na mikakati itakayoboresha Utalii wa kinyumbani.