Huenda sekta ya utalii nchini ambayo ni tegemeo kubwa la uchumi wa nchi ikamiarika zaidi baada ya watalii kuanza kuzuru nchini.
Waziri wa Utalii nchini Najib Balala, amesema Kenya itaendelea kupokea wageni zaidi licha ya mataifa mbalimbali kushuhudia janga la Corona ambalo limekuwa tishio kubwa kote ulimwenguni.
Balala amesema kuwasili kwa watalii 189 humu nchini siku ya Jumamosi ni ishara wazi ya kuanza kuimarika kwa sekta hiyo ambayo imekuwa imedorora kufuatia makali ya janga la Corona.
Kwa upande wake Balozi wa Ukraine nchini Kenya Pravednyk Andrii, amesema serikali ya Ukraine na Kenya zitaendeleza ushirikiano mema ili kuhakikisha uchumi wa mataifa hayo mawili unaboreshwa zaidi.