Picha kwa hisani –
Waziri wa utalii na wanyama pori nchini Najib Balala amemuomboleza mwekezaji katika sekta ya Utalii Kanda ya Pwani Kuldip Sondhi aliyeaga dunia mjini Mombasa.
Balala amemtaja Sondhi kama mwekezaji aliyekuwa na ari ya kuiona sekta ya utalii ikiimarika kila uchao na alichangia pakubwa katika ukuaji wa sekta hiyo katika eneo la Pwani.
Kulingana na Balala Sondhi alikuwa mstari wa mbele katika kuimarisha usafi wa mazingira katika fukwe za Bahari hindi kwa lengo la kuwavutia watalii kuzuru eneo la Pwani.
Sondhi alikuwa mmiliki wa hoteli ya kifahari ya Reef iliyoko eneo la Nyali na vile vile kampuni ya usafiri wa watalii ya Kuldip Safaris.
Amefariki akiwa amepumzika nyumbani kwake eneo la Nyali kulingana na familia yake.