Picha Kwa Hisani –
Waziri wa Utalii nchini Najib Balala amefutilia mbali uteuzi wa Bi Pauline Njoroge kama mwanachama wa mamlaka ya kudhibiti Utalii nchini.
Katika taarifa kwa vyombo habari, Balala amesema uteuzi wa Bi Njoroge umefutiliwa mbali baada ya kubainika wazi kuwa mwaka 2019 alichapisha kwenye mtandao wa kijamii ujumbe wa kuiponda mbuga ya wanyamapori ya Nairobi.
Balala amesema sekta ya utalii haiwezi kufanya kazi na watu walio na mawazo mabaya kuihusu sekta hiyo ambayo inategemewa pakubwa katika kuimarisha uchumi wa taifa hili.
Hatua hiyo ya kufutiliwa mbali kwa uteuzi wa Bi Njoroge kumezua mjadala mkali miongoni mwa wakenya, wakiitaja hatua hiyo kama maonevu.