Wazee hapa Pwani wangali katika hatari ya kuuwawa kwa kutuhumiwa kuwa wachawi.
Kulingana na Shirika linaloangazia maswala ya amani katika Ukanda wa Pwani la KECOSCE chini ya Mkurugenzi wake Bi Phyllis Muema, Wazee hasa katika Kaunti za Kilifi na Kwale wanaishi kwa hofu kubwa ya kuuwawa.
Muema ameonya kuwa iwapo swala hilo tata halitatanzuliwa kupitia kwa Viongozi wa kijamii, kidini na Serikali, basi Wazee katika kaunti za Pwani wataangamizwa wote.
Wakati uo huo, ametaka uongozi wa kaunti hizo kuweka mikakati ya hamasa na amani kwa jamii ili kukomesha hali hiyo.