Story by Ali Chete –
Wazee wa Mvita wamemuidhinisha rasmi mfanyibiashara maarufu Mohamed Masoud Machele kama mgombea wa kiti cha ubunge wa eneo hilo mwaka wa 2022.
Wakiongozwa na Meya wa zamani wa mji wa Mombasa Ahmed Muhdhar, wazee hao wamesema kwa miaka mingi eneo bunge la Mvita limekosa uongozi bora ndiposa wazee hao wamempendekeza Machele kugombea kiti hicho.
Muhdhar amesema iwapo wakaazi wa eneo bunge la Mvita wataamua kwa kauli moja uongozi wa Machele basi eneo bunge hilo litaboreshwa zaidi kimaendeleo na vijana kujengwa uwezo wa kujiimarisha kimaisha.
Kwa upande wake Machele amewashukuru wazee hao kwa kumpendekeza na kuahadi kuwa endapo atachaguliwa kama mbunge wa eneo hilo atatimiza ahadi zake za kuimarisha uchumi.