Baada ya kushuhudiwa kwa ajali za mara kwa mara katika barabara kuu ya Malindi-Magarini kaunti ya Kilifi, sasa Muungano wa sauti ya Wazee wa Mijikenda katika eneo la Malindi na Magarini umedai kupanga siku maalum ya kufanya matambiko katika barabara hiyo.
Kulingana na Msemaji wa Muungano huo Johnson Charo, tambiko hizo ni maombi maalum yatakayosaidia kudhibiti kushuhudiwa kwa ajali katika barabara hiyo kwani idadi kubwa ya wananchi wamepoteza maisha yao.
Wazee hao wamemtaka Gavana wa Kilifi Amason Jefa Kingi kujiunga na Wazee hao katika kufanya tambiko hizo sawia na kuliombea taifa la Kenya.
Kwa upande wake, Katibu mkuu wa Muungano huo Simon Garama, ameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi kuMfuatilia kwa karibu mwanakandarasi anayekarabati barabara katika eneo hilo.