Wazee wa Kaya za wamijikenda wametishia kuwatenga wanasiasa wanaoenda kinyume na maadili ya jamii.
Katika kikao na wanahabari wazee hao wamesema baadhi ya viongozi eneo la pwani wamekua wakirushiana cheche za maneno bila kuiheshimu jamii wanayoiongoza.
Kulingana na mshirikishi wa muungano wa wazee wa kaya Tsuma Kombe tayari wameeka mipangilio ya kufanya mazungumzo ya jinsi watakavyowaonya viongozi wanaoonyesha maadili potovu.
Kwa upande wake mmoja wa wazee hao Erastus Kubo ameelezea hofu yake kwamba huenda vijana wakaiga mienendo ya wanasiasa hao na kupotoka kimaadili.