Muungano wa Wazee wa Kaya wa Mijikenda kanda wa Pwani, umesema tayari mikakati ya kuhakikisha viongozi wa kisiasa hapa Pwani wanabuni chama kimoja cha kisiasa kitakachotambulika nchini inaendelea.
Mshirikishi mkuu wa Muungano huo kanda ya Pwani Tsuma Kombe Nzai, amesema tayari hatua za mwanzo zimefanikiwa ikiwemo kuundwa kwa baraza la wazee litakalo wakilisha kaunti zote 6 za ukanda wa pwani.
Kwa upande wake mmoja wa Wazee hao Erastus Kubo amesema baraza hilo litawashirikisha viongozi mbalimbali wa kisiasa hapa Pwani ili kupata maoni na sera ili kuibuka na mwelekeo wa kisiasa.