Taarifa na Charo Banda.
Wazee wa kaya wameitaka serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya afya kwa kueka mashini za kisasa za kuchunguza ugonjwa wa saratani katika vituo vya afya vya mashinani.
Akizungumza na wanahabari katika kituo cha kitamaduni cha Magarini kule Gongoni mwenyekiti wa wazee wa kaya katika kituo hicho Tsuma Nzai amesema hatua hio itasaidia pakubwa katika kuukabili ugonjwa wa saratani nchini.
Tsuma aidha amesema iwapo wakenya watakumbatia vyakula vya asili sawa na kusitisha uchafuzi wa mazingira wataepuka maradhi mbali mbali ikiwemo saratani.