Story by Ngumbao Jeff-
Wazee wa Kaya katika kaunti ya Kilifi wametoa makataa ya wiki moja kwa wanasiasa na viongozi wa vyama mbalimbali kutoka eneo la Pwani kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuwaunganisha wapwani wote kabla ya uchaguzi.
Wakiongozwa na Emmanuel Munyaya wazee hao wamesema ni sharti viongozi wa Pwani waungane katika chama kimoja ambacho kitabadilisha maisha ya wapwani.
Aidha wameutaka uongozi wa chama cha PAA kushirikiana nao ili wapwani wapate mwelekeo unaofaa kisiasa.
Kwa upande wake Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amesema viongozi wanafaa kujiunga na chama ambacho kitaangazia maslahi ya wakenya na wala sio vyama vya maslahi.
2 Attachments