Picha kwa Hisani –
Wazee wa Kaya eneo la Pwani sasa wanaitaka serikali kupitia Wizara ya Afya nchini kuidhinisha dawa za miti shamba kuwa miongoni mwa dawa za kutibu virusi vya Corona.
Wazee hao wa Kaya Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Abdallah Mnyenze amesema virusi vya Corona vinawezakutiwa na dawa za kienyeji badala ya kutegemea dawa zilizo na gharama ya juu.
Naye Mzee Stanley Kenga ameitaka serikali kutambua ushauri wa wazee nchini ili kuzindua tiba asili ya kukabiliana na virusi vya Corona kwani tiba asili inatambulika kote dunia.
Kwa upande wake Mshirikishi wa Wazee wa Kaya Tsuma Nzai Kombe, amevitaja virusi vya Corona kama maradhi ya kivuti, akisema yanaweza kutibiwa kwa kutumia mitishamba.
Hata hivyo wazee hao wa Kaya wameyazungumza hayo baada ya kufanya tambiko la kuiombea nguvu miti shamba.