Story by: Mercy Tumaini
Chama cha Wazee wa Kaya za Mijikenda kanda ya Pwani kimewataka viongozi waliochaguliwa kuwaheshimu wazee wa Kaya na wala sio kuwatumia wazee hao kama mbinu ya kujinufaisha binafsi.
Msemaji wa Chama hicho Naomi Cidi Kumbatha amesema Wazee wa Kaya wamekuwa wakidharauliwa na viongozi wa kisiasa na kuwatumia wakati wanapotafuta nyadhfa za kisiasa.
Akihutubia Wanahabari katika msitu wa Kayafungo, Naomi amesema wazee hao watawasilisha mapendekezo yao wenyewe mbele ya Rais kwani viongozi wa kisiasa wamekuwa wakiwalaghai kwa miaka mingi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho cha wazee wa Kaya za Mijikenda Mwinyi Mwalimu Murisho amesema changamoto wanazopitia wazee hao ni ukosefu wa hati miliki na kutotambuliwa na serekali.