Taarifa na Charo Banda.
Wazee wa Kaya za Mijikenda kule Malindi kaunti ya Kilifi wanahofia kufurushwa katika makao ya kitamaduni katika kituo cha kitamaduni cha MADCA, baada ya bwenyenye mmoja kwa jina Josphat Charo Noti kudai kuwa ardhi wanaoendeleza shuhuli zao ni yake.
Akiongea na wanahabari kule mjini Malindi, Katibu wa chama cha wilaya ya Malindi MADCA, Joseph Mwarandu amesema ardhi hiyo wameishi kwa takribani miaka 14 na kuna wazee 50 ambao wamekuwa wakiwahifadhi.
Kwa upande wake mmoja wa wazee hao Kazungu wa HaweRisa, amesema kituo hicho kimekuwa tegemeo kubwa kwa serikali na wanafunzi katika maswala ya historia za utamaduni, lakini sasa itakuwa changamoto kwao.
Wazee hao sasa wanaitaka serikali kuingilia kati swala hilo na kuhakikisha linalitatua kwa haraka ili kuwawezesha wazee hao kuishi kwa amani.