Wazee 85 wameuwawa kwa tuhuma za uchawi katika kaunti ya Kilifi kwenye kipindi cha mwaka mmoja uliopita utafiti uliofanywa na shirika la KECOSE umebaini.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Phyllis Muema amesema Wazee hao waliuwawa katika maeneo ya Bamba, Magarini, Ganze, Rabai na Kaloleni kati ya mwezi Juni mwaka uliyopita na mwezi Juni mwaka huu.
Akizungumza na Wanahabari, Phyllis amesema takwimu hizo zinatisha na kuna haja ya kaunti ya Kilifi kuekeza zaidi katika mikakati ya amani na hamasa kwa vijana wanaohusika na uovu huo.
Aidha amesema hali ni sawia na kaunti ya Kwale hasa maeneo ya Kinango ambako wazee wawili huuwawa kila juma kwa tuhuma hizo za uchawi, na akasisitiza jitihada zaidi kuidhinishwa ili kuidhibiti hali hiyo.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.