Afisa wa miradi katika shirika la kijamii la KECOSCE, Hassan Kibwana amesema ni aibu kwa wazazi kuwaona watoto wao kama mzigo msimu huu wa likizo ndefu ya mwisho wa mwaka.
Kibwana amewakosoa wazazi kwa kutojishughulisha na hali za watoto wao hasa msimu huu ambapo wengi wao wako nyumbani kwa likizo.
Kibwana amewataka viongozi wa kidini kujitolea katika kuwaelekeza watoto katika njia njema ili kuwakinga na maovu na kupoto maadili.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.