Kamishina wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki amewataka wazazi kutahadhari masomo yanayotolewa kwa watoto wao msimu huu wa likizo akisema baadhi yanawafundisha watoto masuala ya itikadi kali.
Kulingana na Achoki makundi ya kihalifu yanatumia njia hiyo kuwanasa vijana kuendeleza elimu yao ya itikadi kali.
Akiongea mjini Mombasa Achoki amewataka wazazi kushirikiana na idara ya usalama hasa vijana wao wanapoahidiwa kazi katika mataifa ya kigeni akisema baadhi zinatumika kuendeleza uhalifu.
Taarifa na Hussein Mdune.