Wizara ya elimu katika kaunti ya Kwale imewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanaendeleza masomo wakiwa nyumbani wakati huu ambapo shule zimefungwa mapema kufuatia tishio la maambukizi ya virusi vya Corona.
Katika mahojiano na wanahabari waziri wa elimu katika kaunti hio Mangale Chiforomodo amesema hali hio itawasaidia wanafunzi kutosahau waliofundishwa shuleni.
Chiforomodo aidha amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao njia zitakazowasaidia kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
Chiforomodo amefichua kwamba tayari maafisa wa serikali ya kaunti hio wameelimishwa kuhusu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo.