Story by Hussein Mdune-
Mgombea wa kiti cha uwakilishi wadi ya Kinango katika kaunti ya Kwale kwa tiketi ya chama cha UDM Isaac Beja Bora, amewahimiza wazazi wa wadi hiyo kuzingatia elimu ya watoto wao ili kuwajenga uwezo katika siku za usoni.
Beja amesema ni kupitia elimu ndipo familia zisizojiweza katika jamii zitanufaika maishani.
Mwanasiasa huyo ameahidi kuboresha swala la elimu kwa kuwasaidia watoto wanaotoka katika familia zisizojiweza kujiunga na vyuo vya kiufundi ili kupata ujuzi mbalimbali.
Wakati uo huo amewataka wazazi kuwa karibu mno na watoto wao wakati huu wa likizo huku akiwataka wakaazi wa wadi hiyo kudumisha amani.
Kiongozi bora mwenye maono mazuri kwa wadi ya kinango… Kiongozi Beja Bora amesaidia Wakwale wengi kupitia miradi mingi ya kuendelea wanajamii walio katika hali za umaskini… Kiongozi Beja tunamtambua kwa uchapakazi wake alipokua mwenyekiti wa CBO, Afisa wa Shirika la Plan International, nk. Matunda yake tunayaona..
#Aliweza na anaweza…. Kinango ya kiongozi Bora… Kura kwa Beja Bora 💪