Wazazi katika Kaunti ya Kwale wamepewa wito kuhakiksha kuwa wanawapa watoto wao vifaa vya kutosha ili kuwawezesha kuendelea na masomo yao ya Muhula wa kwanza mwaka huu.
Kulingana na Mkurugenzi wa elimu katika Kaunti ya Kwale Martin Cheriyot, Shule zimefunguliwa kulingana na maagizo ya Wizara ya elimu na kalenda ya mosomo ya mwaka mpya wa 2021.
Cheriyot amesema kuwa wazazi hapaswi kulalamikia muda mfupi waliostahili kutayarisha wanafunzi kwa muhula mpya kufuatia kuwa mipango hiyo imetokana na Wizara ya Elimu kutaka kufidia muda uliopotea kufuatia Janga la Corona .
Aidha, Mkurugenzi hyuo wa Elimu amesema iwapo mzazi anakumbwa na changamoto za karo itakuwa vyema afanye mazungumzo na usimamizi wa shule ili kukubaliana ni vipi atakamilisha karo ili kumuwezesha mwanafunzi kusalia Shuleni .