Wazazi ambao watoto wanajihusisha na vitendo vya kihalifu katika eneo la Kisauni Kaunti ya Mombasa wamehimizwa kuwafichua kwa maafisa wa polisi ili warekebishwe badala ya kuendelea kuwahangaisha wakaazi.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kijamii la Kenya Community Support Centre hapa Pwani Bi Phyllis Muema amesema kwamba msukosuko wa kiusalama unaolikumba Gatuzi hilo dogo la Kisauni umechangiwa na hali ya Wazazi kuwaficha watoto wao wanaojihusisha na uhalifu.
Akizungumza katika eneo la Kisimani huko Kisauni, Bi Muema amesema kwamba ikiwa wazazi wangekuwa wazi kuhusiana na tabia za wanao basi hali hiyo ingethibitiwa mapema na hali ya Vijana wenye umri mdogo kusajiliwa katika magenge ya kijambazi ingekomeshwa.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.