Story by Hussein Mdune–
Afisa mkuu wa vyuo vya kiufundi katika eneo la Samburu kaunti ya Kwale Jennifer Isama amewasihi wazazi ambao watoto wao hawajafanikiwa kujiunga na shule za upili kuhakikisha wanajiunga na vyuo vya kiufundi.
Jennifer amesema hatua ya wazazi kudharau masomo ya kiufundi imechangia watoto wengi kupitia changamoto za maisha.
Amesema ni kupitia ujuzi aina mbalimbali ndipo utaimarisha maisha ya watoto hao sawa na kujitenga na visa vya uhalifu.
Wakati uo huo ameweka wazi kwamba vijana wengi wamejikuta katika makundi ya kihalifu na utumizi wa mihadarati kufuatia ukosefu wa ajira, akisisitiza umuhimu wa elimu ya kiufundi.