Mwakilishi wa wadi ya Magarini kaunti ya Kilifi Elina Mbaru amesema kuna haja ya ushirikiano baina ya wananchi, walimu pamoja na wadau wa sekta ya elimu ili kuboresha sekta hiyo eneo hilo la Magarini.
Kulingana na Mbaru, sekta ya Elimu ndio uti wa mgongo kimaendeleo kwa mwananchi, hivyo kuna haja ya kuimarishwa hata zaidi.
Kiongozi huyo aidha amewapa changamoto maafisa wa elimu eneo hilo kuhakikisha kwamba wanawajibikia majukumu yao ipasavyo badala ya kukaa kwa maofisi bila ya kujua na kufahamu kuhusu changamoto wanazopitia wanafunzi.
Ameongeza kuwa atashirikiana kwa karibu na vitengo vyote kwa lengo la kuimarisha matokeo ys mitihani ya kitaifa kwa wanafunzi akidai ni kupitia hatua hiyo ambapo jamii itasonga mbele kimaendeleo.
Taarifa na Dominick Mwambui.