Story by Hussein Mdune
Mkurugenzi wa elimu katika gatuzi dogo la Samburu Bernad Salim amewataka wakaazi kulitilia mkazo swala la elimu.
Kulingana na Salim licha ya familia nyingi kupitia changamoto za maisha viwango vya elimu vitaimarika katika eneo hilo iwapo wazazi watawajibikia majukumu yao.
Amesema eneo la Samburu linapitia changamoto nyingi za kielimu huku akitilia mkazo umuhimu wa elimu mashinani.
Wakati uo huo amewahimiza wakaazi wa eneo hilo kushirikiana na wadau wa elimu ili kuimarisha viwango vya elimu.