Askofu wa Kanisa la Tazama Christ United Methodist, Bernard Mudiri amesema wazazi hapa Pwani wanapaswa kukubali shtuma wanazopewa kufuatia kuathirika kwa watoto wao na swala la itikadi kali, na ugaidi.
Askofu Mudiri amesema uzembe wa wazazi ndio umechangia pakubwa katika kudidimia kimaadili kwa watoto hali inayowaweka katika hatari ya kujiunga na makundi ya kigaidi.
Akizungumza huko Mtwapa kaunti ya Kilifi, Askofu Mudiri amesema wazazi watajilaumu wenyewe kwa kutokuwa na muda na watoto wao, katika kuwashauri na kuwakinga na maswala ya itikadi kali na ugaidi.
Kiongozi huyo wa kidini amedokeza kuwa ni lazima Wazazi, Viongozi wa kidini na jamii kwa jumla kuwaelekeza watoto katika njia njema, ili wayafichue walionayo kwa lengo la kuwasaidia kimawazo na kimaisha.