Picha kwa hisani –
Serikali imewahakikisha wazazi na wadau wengine kwamba mikakati ya maandalizi ya shule imeimarishwa zaidi na wanafunzi wanafaa kurudi shule kuanzia siku ya Jumatatu hapo kesho.
Katika kikao na Wanahabari kule jijini Nairobi, Waziri wa Elimu nchini Profesa George Magoha amesema mikakati yote iko sawa na wazazi hawafai kuhofia kuhusu usalama wa watoto wao kwani virusi vya Corona vimedhibitiwa shuleni.
Waziri Magoha amesema tayari zaidi ya madawati elfu tano yamekamilika na yatasambazwa shuleni huku akisema shilingi bilioni nne kufikia kesho zitakuwa zimesambazwa katika shule za msingi na bilioni 16 kwa shule za upili.
Kwa upande wake Waziri wa uchukuzi nchini James Macharia, amesema mazungumzo baina ya serikali na wadau wa sekta ya uchukuzi yamefanywa na kuafikia kwamba madereva wote hawatahitaji kusafiri kwa mwendo mrefu na watapimwa kubaini iwapo wametumia vileo .
Hata hivyo mawaziri hao yameyasema hayo baada ya kufanya mkutano na wadau wa maswala ya kielimu ikiwemo Tume ya TSC, Chama cha walimu nchini KNUT, chama cha wazazi nchini pamoja na chama cha walimu wa shule za kibinafsi miongoni mwa wadau wengine.