Story by Charo Banda –
Hali ya sintofahamu imetanda katika shule ya upili ya Wavulana ya Malindi High kaunti ya Kilifi baada ya wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo kupiga kambi katika lango kuu la shule hiyo wakitaka kujua hatma ya watoto wao baada ya bweni la shule hiyo kuchomeka.
Wakizungumza na Wanahabari, mmoja wa wazazi hao Kaingu Rembo amesema hawatabanduka katika lango la shule hiyo hadi pale watakapopewa fursa ya kuzungumza na watoto wao.
Naye Julia Ogona amesema licha ya kurauka katika shule hiyo baada ya bweni la shule hiyo kuchomeka usiku wa kuamkia leo hawajapewa nafasi ya kuwaona watoto wao.
Hata hivyo maafisa wa zima moto kutoka mjini Malindi walifika katika shule hiyo na kuuzima moto huo.