Mbunge wa Voi Johnes Mlolwa amewataka wazazi wa kiume katika eneo hilo kuwajibikia majukumu yao vyema badala ya kuwaachia wazazi wa kike majukumu ya familia.
Akizungumza katika kikao na wazee wa eneo la Ndome mjini Voi, Mlolwa amesema ni jukumu la kila mtu kujihusisha na shughuli za kulijenga taifa hili hasa kwa kuwajibikia majukumu yao.
Mlolwa amesema kuwepo na idadi ndogo ya wanafunzi shuleni imechangiwa na wazazi wa kiume kukwepa majukumu yao ya familia.
Wakati uo huo ameahidi kama viongozi wa kaunti hiyo wataungana ili kuhakikisha swala la kupunguzwa kwa maeneo bunge hasa yale ya kaunti ya Taita taveta linasuluhishwa kwa usawa.
Taarifa na Fatuma Rashid.