Wazazi na wanafunzi wa Kaunti ya Lamu wamehakikishiwa usalama wa kutosha wakati huu ambapo muhula wa kwanza umeanza rasmi.
Kamishna wa Kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema swala la usalama limezingatiwa akiwataka wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni kwani mazingira ya shule yana ulinzi wa kutosha.
Macharia amesema Idara ya usalama imeimarisha doria kila pembe ya Kaunti hiyo ili kuhakikisha shughuli za kila siku zinaendelea bila ya wasiwasi wowote.
Wakati uo huo, Wakaazi wa Boni Kaunti ya Lamu wamedinda kuwapeleka watoto wao shuleni licha ya amri kutoka kwa Mshirikishi mkuu wa utawala Kanda ya Pwani John Elungata kuwataka Wazazi hao kuwapeleka shuleni kwani shule zilizofungwa tangu mwaka 2014 zimefunguliwa.