Kituo cha Radio Kaya kilijiunga na wadau wengine katika kampeni ya kuhamasisha wazazi pamoja na wanafunzi wa Mwanguda kule Lungalunga katika kaunti ya Kwale kuhusu hedhi salama.
Katika kampeni hiyo zaidi ya wazazi 500 na wanafunzi wa Kike 600 kutoka eneo hilo wamepata mafunzo hayo ya hedhi salama, mafunzo ambayo pia yamejumuisha wanafunzi wa Kiume.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mama wa kaunti ya Kwale Bi Christine Mvurya amewataka wazazi wa kaunti hiyo kutenga fedha za kuwanunulia watoto wao vitambaa vya sodo.
Bi Christine amesema wakati ni sasa kwa wazazi kuzungumza na watoto wao waziwazi kuhusu masuala ya hedhi, akisema wasichana wanaovunja ungo hupitia changamoto nyingi kutokana na uoga kwa kulizungumzia swala hilo.