Kamishna wa Kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amewalaumu wazazi na jamii ya kaunti ya Kwale kwa ujumla kwa kukosa kuwajibikia vyema majukumu ya ulezi kwa wanao.
Akiongea na mwanahabari wetu Ngumo amesema kuwa juhudi za idara ya usalama ikishirikiana na wadau mbali mbali kuhimiza wazazi kulipa kipaumbele suala la malezi ya wanao hazijafua dafu.
Ngumo amekariri kwamba ni kupitia malezi mema na muongozo mwema kutoka kwa wazazi, watoto watawezeshwa kufaulu maishani.
Kiongozi huyo vilevile amewataka wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wao ili kuwaepusha na uhalifu,utumizi wa mihadarati miongoni mwa tabia zengine zisizofaa.
Taarifa na Mariam Gao.