Wazazi walio na watoto walemaavu katika maeneo ya Mkomani, Junju, Shauri moyo na Kibaoni kaunti ya Kilifi wameitaka serikali kupitia idara husika kuwaangazia watoto wanaoishi na ulemavu katika eneo hilo.
Akiongea na wanahabari wakati wa uzinduzi wa muungano wa kutetea haki za walewavu wa Shauri Moyo Mercy for Angels, mwenyekiti wa muungano huo Magret Uchi amesema kuwa walemavu katika maeneo hayo hulazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta huduma mbali mbali ikiwemo za kiafya.
Kwa upande wake afisa wa baraza la kitaifa la watu wanaoishi na ulemavu kaunti ya Kilifi Mathias Mwatsuma Tsuma amewataka walemavu kujitokeza na kusajiliwa ili wanufaike na misaada mbali mbali kutoka kwa serikali.
Taarifa na Marieta Anzazi.