Picha kwa hisani –
Himizo zimezidi kutolewa kwa wazazi wa kaunti ya kwale kujitahidi kuhakikisha watoto wao wanarejea shuleni ifikapo januari mwaka ujao, ili kuendelea na masomo yao pasi na changamoto.
Mkurugenzi wa shirika la kielimu kaunti hiyo la KWEA Bi Sabina Saiti, amesema licha ya kuwa watoto wengi wamepitia changamoto nyingi ikiwemo kupachikwa ujauzito katika kipindi hiki cha likizo ndefu iliyo sababishwa na janga la korona wanahaki ya kurudi shuleni ili kutimiza ndoto zao maishani.
Wakati uo huo bi Sabina amewataka wazazi kuweza kuishinikiza serikali kuu kuajiri maafisa wa kutoa ushauri nasaha mashuleni akisema watoto wengi hasa waliopitia dhulma mbalimbali wameathirika kisaikolojia .
Ameitaja hali hiyo kama itakayosababisha changamoto kwa watoto hao kuweza kurudi katika hali zao za kawaida kimasomo.