Mshirikishi mkuu wa Utawala kanda ya Pwani John Elanguta amewataka machifu na manaibu wao pamoja na wazazi katika eneo la Magarini kuhakikisha watoto wote waliomaliza darasa la nane wanajiunga na kidato cha kwanza.
Elungata amesema asilimia 64 ya wanafunzi waliokalia mtihani wa KCPE wamesalia nyumbani licha ya agizo la serikali kuwa kila mwanafunzi anafaa kuripoti shuleni.
Akiongea na wadau wa sekta ya elimu eneo la Magarini kaunti ya Kilifi, Elungata amesema serikali itawanasa na kuwashtaki wazazi wote na machifu ambao watakaidi amri hiyo kufikia juma lijalo.
Wakati uo huo ameigiza idara ya polisi kuwakamata walimu wote wanaoitisha pesa za ziada kwa wanafunzi, mbali na agizo la serikali ili kukomesha uovu huo.
Taarifa na Charo Banda.