Wadau wa sekta ya uvuvi kanda ya Pwani wameitaka Mamlaka ya Baharini KMA kuyafanyia ukarabati maboya yanayoelekeza usalama wa baharini katika sehemu ya Mtangawanda katika kaunti ya Lamu.
Kulingana na Katibu wa Muungano wa Wavuvi Pwani Anwar Abae, maboya hayo yamemaliza takribani wiki mbili tangu yaharibike na hakuna juhudi zozote za ukarabati zimetekelezwa.
Ametaja hatua hiyo kama inayo hatarisha maisha ya wavuvi wengi ambao wanatumia sehemu hizo.
Wakati uo huo ametaja kuwa usalama wa baharini umedorora kwa kiwango kikubwa kutokana na kukosekana kwa mataa baharini na kutatiza usafiri na hata sekta ya uvuvi.
Taarifa na Hussein Mdune.