Taarifa na Ephie Harusi.
Kilifi, Kenya, Julai 12 – Wavuvi katika kaunti ya Kilifi wameonywa dhidhi ya matumizi ya vifaa vya uvuvi vinavyoharibu mazingira ya baharini.
Akiongea na wanahabari mjini Kilifi, Afisa mkuu wa mazingira katika gatuzi la Kilifi Maryam Jenneby amesema kuwa wizara yake itashirikiana na wizara ya uvuvi ya Kilifi pamoja na serikali ya kitaifa ili kupitisha sheria inayopania kuchukulia hatua wavuvi wanaotumia vifaa vinavyo haribu mazingira ya bahari.
Aidha maoni hayo yameungwa mkono na mkurugenzi wa mazingira katika kaunti ya kilifi Bi Zena Hasssan, kwa kusema kua ni sharti viwanda vyote vinavyotoa maji taka baharini vitimize sheria na viwango vya kimazingira vinavyotakikana ili kuzuia uchafuzi wa maji baharini.