Taarifa na Charo Banda.
Malindi Kenya, Juni 8 – Wavuzi katika eneo la Cha fisi huko Watamu kaunti ya kilifi sasa wametakiwa kufuatia sheria za uvuvi ili kukomesha mizozo ya mara kwa mara baina yao na maafisa wa shirika la KWS katika eneo hilo.
Hii ni baada ya kubainika kuwa asilimia kubwa ya wavuvi katika fuo za bahari ya hindi wanashiriki uvuvi haramu na ambao haukubaliki na KWS.
Akiongea na takriban wavuvi 300 mbunge wa Kilifi kazkazini Owen Baya amesema kuwa wavuvi wengi katika eneo hilo wamekuwa wakinaswa na maafisa wa KWS kwa kutumia vifaa bandia kuvua samaki.
Kulingana na afisaa mkuu wa KWS tawi la Watamu Daddly Tsinyau wavuvi wengi eneo hilo hawazingatii uvuvi unaofaa na kwamba hutumua nyavu bandia ambazo zinaathiri vibaya mazingira.