Mwenyekiti wa Muungano wa wavuvi Pwani Anwary Abae ameitaka Mamlaka ya ubaharia nchini KMA kuwapa vifaa vya mawasiliano wavuvi hasa kipindi hiki mvua inaposhuhudiwa kunyesha.
Kulingana na Abae, huenda kukashuhudiwa mawimbi makali baharini kutokana na upepo mkali na mvua nyingi inayoshuhudiwa hivyo basi ni vyema iwapo watapewa vifaa hivyo.
Akizungumza na Wanahabari, Abae amewataka wavuvi kuwa makini zaidi wanapokuwa kwenye shughuli zao za uvuvi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo nchini, George Magoya amesema tayari Mamlaka hiyo imezindua mpako maalum wa kupeleka mitambo ya Satellite kufuatilia meli na vifaa vyengine vya baharini ili kukabiliana na majanga. Haya yanajiri baada ya wavuvi 14 kuokolewa na jeshi la majini baada ya Mashua zao kuzama maji walipokuwa kwenye shuhuli zao za uvuvi katika eneo la Kiunga kaunti ya Lamu.
Taarifa na Hussein Mdune.