Wavuvi Katika eneo la Malindi Kaunti ya kilifi wamelalamikia vikali uhaba mkubwa wa samaki Katika eneo Hilo Hali ambayo imepelekea Wavuvi wengi kusalia bila ajira kwa sasa.
Wakiongozwa na Ali Salim Ali,wavuvi hao wamesema hali hiyo imechangiwa na baadhi ya wavuvi kutoka nchi za kigeni ambao wanaendeleza uvuvi haramu katika eneo hilo.
Jamil Athman Omar ambaye pia ni mmoja wa wavuvi katika eneo hilo amedai kwa sasa shughuli zote za uvuvi eneo hilo zimesambaratika,akiongeza kuwa serikali inafaa kuchunguza upya leseni za wavuvi wa kigeni humu Nchini.