Story by Our Correspondents-
Takriban wavuvi 5 kutoka eneo la Shimoni katika eneo bunge la Lungalunga kaunti ya Kwale wanazuiliwa nchini Somalia katika mji wa Mudoa yapata wiki mbili sasa.
Wavuvi hao ambao wanazuiliwa na maafisa wa polisi nchini humo wamedai hatua hiyo imejiri baada ya kutoelewana na muajiri wao anayetaka kulipwa fidia ya shilingi laki moja kabla ya kuwaruhusu kurudi nyumbani.
Wakiongozwa na Mohamed Omari Mgala, Wavuvi hao ambao walipata nafasi ya kuzungumza kwa njia ya simu, wamesema wanaishi katika mazingira magumu tangu kukamatwa kwao na kuitaka serikali kuingilia kati swala hilo ili warudi nyumbani.
Wavuvi hao ambao wanadaiwa kuwa 12 wengine kutoka maeneo mengine ya kanda ya Pwani ni pamoja na Omari Shee, Hamisi Zito, Kimosha Abdallah na Abdallah Gwashe ambao walikuwa wameenda Somalia kuendeleza shughuli za uvuvi kupitia usimamizi wa mfanyibiashara mmoja maarufu kutoka kaunti ya Lamu.