Story by Salim Mwakazi-
Wavuvi katika maeneo ya Shimoni na Vanga eneo bunge la Lungalunga kaunti ya Kwale, wameitaka serikali ya kitaifa kupitia idara husika kuwaelimisha kuhusu sheria mpya za uvuvi.
Wakiongozwa na Mohamed Ferunzi, wavuvi hao wamesema kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa shughuli zao za uvuvi zimetatizika baada ya kuzuiliwa na walinzi wa baharini kwa madai ya kuendeleza uvuvi haramu.
Wavuvi hao wamesema hatua hiyo imetokana na ukosefu wa ufahamu wa sheria mpya za uvuvi miongozi mwao, hali ambayo imewafanya kuhangaishwa wanapoendeleza shughuli zao za uvuvi.
Wavuvi hao wanasema wanategemea pakubwa sekta ya uvuvi kujikimu kimaisha na kwamba ni lazima utata huo usuluhishwe ili waendeleze shughuli zao bila ubaguzi.